Al-Baqara 2:166
البقرةإِذْ تَبَرَّأَ ٱلَّذِينَ ٱتُّبِعُوا۟ مِنَ ٱلَّذِينَ ٱتَّبَعُوا۟ وَرَأَوُا۟ ٱلْعَذَابَ وَتَقَطَّعَتْ بِهِمُ ٱلْأَسْبَابُ
Waliofuatwa watakapowakataa wale waliowafuata, na hali ya kuwa wamekwishaiona adhabu; na yatakatika kabisa mafungamano yao.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Walio fuatwa watakapo wakataa wale walio wafuata, na hali ya kuwa wamekwisha iona adhabu; na yatakatika mafungamano yao. [166]
[166] Siku hiyo wafuasi watatamani wakubwa wao wawaokoe na upotofu, nao watawakataa na kujitenga nao wakisema: Hatukukwiteni mtut'ii katika kumuasi Mola wenu Mlezi. Hilo ni pumbao lenu tu na uovu wa vitendo vyenu. Makhusiano baina yao na mapenzi waliyo kuwa nayo duniani yatakatika siku hiyo, na watakuwa maadui wao kwa wao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Watakapoiyona adhabu ya Akhera, watajitenga wale viongozi waliofuatwa kujiepusha na wale waliowafuata katika ushirikina na zitawakatikia wao aina zote za mawasiliano waliyojifungamanisha nayo duniani: ya ujamaa, ufuasi, dini na mengineyo yasiyokuwa hayo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net