Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 165

Al-Baqara 2:165

البقرة

وَمِنَ ٱلنَّاسِ مَن يَتَّخِذُ مِن دُونِ ٱللَّهِ أَندَادًا يُحِبُّونَهُمْ كَحُبِّ ٱللَّهِ ۖ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ أَشَدُّ حُبًّا لِّلَّهِ ۗ وَلَوْ يَرَى ٱلَّذِينَ ظَلَمُوٓا۟ إِذْ يَرَوْنَ ٱلْعَذَابَ أَنَّ ٱلْقُوَّةَ لِلَّهِ جَمِيعًا وَأَنَّ ٱللَّهَ شَدِيدُ ٱلْعَذَابِ

Maana

Na katika watu wapo wanaojifanyia waungu wasio kuwa Mwenyezi Mungu. Wanawapenda kama kumpenda Mwenyezi Mungu. Lakini walioamini wanampenda Mwenyezi Mungu zaidi sana. Na laiti waliodhulumu wakajua watakapoiona adhabu kuwa nguvu zote ni za Mwenyezi Mungu, na kuwa Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu!

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na katika watu wapo wanao chukua waungu wasio kuwa Mwenyezi Mungu. Wanawapenda kama kumpenda Mwenyezi Mungu. Lakini walio amini wanampenda Mwenyezi Mungu zaidi sana. Na laiti walio dhulumu wakajua watakapo iona adhabu kuwa nguvu zote ni za Mwenyezi Mungu na kuwa Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu! [165]

[165] Na juu ya dalili zilio wazi baadhi ya watu walio potelewa na akili wamewafanya miungu mingine isiyo kuwa Mwenyezi Mungu, wakiwat'ii na kuwaabudu kama Mwenyezi Mungu na wakawafanya mfano wa Mwenyezi Mungu. Muumini humuelekea Mwenyezi Mungu tu, na kumt'ii kwake hakuna ukomo. Ama hao ut'iifu wao kwa miungu yao hulegalega wakati wa shida. Hapo basi humkimbilia Allah Subhanahu. Na walio jidhulumu nafsi zao lau wangezingatia adhabu itakayo wapata Siku ya Malipo, utakapo dhihiri Ufalme wa Mwenyezi Mungu, na ut'iifu ukawa wake tu wangeli achilia mbali ukhalifu wao na wangeli sita kutenda dhambi zao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Pamoja na hizi hoja za kukata, kinatoka kikundi cha watu wakichukua, badala ya Allah Mtukufu, masanamu na wategemewa wakiwafanya ni kama Allah Mtukufu na kuwapa mapenzi, heshima na twaa, Mambo yasiyostahiki kufanyiwa isipokuwa Allah Mtukufu Peke Yake. Na Waumini, mapenzi yao kwa Allah Mtukufu ni makubwa zaidi kuliko mapenzi ya hawa makafiri kwa Allah Mtukufu na kwa waungu wao. Sababu Waumini wamemtakasia Allah Mtukufu mapenzi yao yote. Na hao makafiri wamemshirikisha Allah Mtukufu katika mapenzi. Na lau wangalijua wale waliojidhulumu nafsi zao kwa kumshirikisha Allah Mtukufu katika maisha ya kidunia, pindi watakapoiona adhabu ya Akhera, kwamba Allah Mtukufu Ndiye Peke Yake Mwenye nguvu zote na kwamba Allah Mtukufu ni mkali wa adhabu, hawangaliwafanya wasiokuwa Allah Mtukufu kuwa ni waungu wakawa wanawaabudu, badala ya Allah Mtukufu, na kujikurubisha nao Kwake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net