Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 167

Al-Baqara 2:167

البقرة

وَقَالَ ٱلَّذِينَ ٱتَّبَعُوا۟ لَوْ أَنَّ لَنَا كَرَّةً فَنَتَبَرَّأَ مِنْهُمْ كَمَا تَبَرَّءُوا۟ مِنَّا ۗ كَذَٰلِكَ يُرِيهِمُ ٱللَّهُ أَعْمَـٰلَهُمْ حَسَرَٰتٍ عَلَيْهِمْ ۖ وَمَا هُم بِخَـٰرِجِينَ مِنَ ٱلنَّارِ

Maana

Na watasema wale waliofuata: 'Laiti tungeweza kurudi tukawakataa wao kama wanavyotukataa sisi!' Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu atakavyowaonyesha vitendo vyao kuwa majuto yao; wala hawatakuwa wenye kutoka Motoni.[1]

[1] Basi matendo yao (ya kumwabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu Mmoja) yakapotelea mbali. Na hali zao zikaangamia, na ikawadhihirikia kuwa wao walikuwa ni waongo. Na kwamba matendo yao waliyoyatarajia yawanufaishe na wapate matokeo yake yaliwabadilikia yakawa masikitiko na majuto.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na watasema wale walio fuata: Laiti tungeweza kurudi tukawakataa wao kama wanavyo tukataa sisi! Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu atakavyo waonyesha vitendo vyao kuwa majuto yao; wala hawatakuwa wenye kutoka Motoni. [167]

[167] Na hapa wafuasi itawabainikia kuwa walipotea walipo wafuata viongozi wao katika upotovu, na watatamani warejee duniani wawakatae viongozi wao kama wao walivyo wakataa siku ya leo. Vitendo vyao viovu vitadhihiri wajute, lakini wapi! Vimekwisha watumbukiza Motoni, na wala hawatatoka humo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na wale wafuasi watasema, «Twatamani tuwe na marejeo ya duniani, ili tutangaze kujitenga kwetu na hawa viongozi kama walivyotangaza kujitenga kwao na sisi.» Na kama Alivyowaonesha Allah Mtukufu ukali wa adhabu Yake, Siku ya Kiyama, Atawaonesha vitendo vyao viovu kuwa ni majuto kwao. Na hawatakuwa ni wenye kutoka Motoni kabisa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net