Al-Baqara 2:163
البقرةوَإِلَـٰهُكُمْ إِلَـٰهٌ وَٰحِدٌ ۖ لَّآ إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ٱلرَّحْمَـٰنُ ٱلرَّحِيمُ
Na Mungu wenu ni Mungu mmoja tu, hapana mungu ila Yeye. Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na Mungu wenu ni Mungu mmoja tu, hapana mungu ila Yeye. Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu. [163]
[163] Hakika Mungu wenu anaye stahiki kuabudiwa pekee ni Mmoja. Hakuna mungu mwenginewe, wala hapana utawala ila wake. Tena Yeye amesifika kuwa ni Mwenye rehema, basi Yeye ni Rahim, Mwenye Kuwarehemu waja wake katika kuwaumba na kuwafanya walivyo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na Mola wenu, enyi watu, ni Mola Mmoja Aliyepwekeka katika dhati Yake, majina Yake, sifa Zake na vitendo Vyake na uja wa viumbe Vyake Kwake. Hapana apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Yeye, Mwingi wa rehema, Mwenye kusifika kwa sifa ya rehema katika dhati Yake, vitendo Vyake kwa waja Wake wote, na Mwenye kuwarehemu waumini.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net