Al-Baqara 2:162
البقرةخَـٰلِدِينَ فِيهَا ۖ لَا يُخَفَّفُ عَنْهُمُ ٱلْعَذَابُ وَلَا هُمْ يُنظَرُونَ
Watadumu humo. Hawatapunguziwa adhabu wala hawatapewa muda wa kupumzika.[1]
[1] Hawatapumzishwa, yaani kupewa muhula, kwa sababu wakati wa muhula ambao ulikuwa duniani ulikwishapita.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Watadumu humo. Hawata-punguziwa adhabu wala hawatapewa muda wa kupumzika. [162]
[162] Na wataendelea katika laana hii na katika Moto, wala hawatapunguziwa adhabu, wala hawatapewa muhula wala haitoakhirishwa. Hata wakiomba muhula na kuakhirishwa hawataitikiwa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Watadumu kwenye laana na Moto. Hawatapunguziwa adhabu, wala hawatapumzishwa na kungojewa kwa udhuru wowote watakaoutoa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net