Al-Baqara 2:15
البقرةٱللَّهُ يَسْتَهْزِئُ بِهِمْ وَيَمُدُّهُمْ فِى طُغْيَـٰنِهِمْ يَعْمَهُونَ
Mwenyezi Mungu atawadhihaki na atawaacha katika upotovu wao wakitangatanga ovyo.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Mwenyezi Mungu atawadhihaki wao na atawawacha katika upotofu wao wakitangatanga ovyo. [15]
[15] Mwenyezi Mungu Subhana atawalipa kwa huko kudhihaki kwao, na atawaandikia uangamifu unao lingana na hayo maskhara yao na dharau zao. Atawatendea inavyo stahili kutendewa mwenye kudhihaki, na anawapa muhula tu katika dhulma yao iliyo ovu, inayo watia upofu wasiione haki. Kisha khatimaye ndipo atapo watia mkononi kwa adhabu yake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Allah Mtukufu anawacheza shere wao na kuwapa muhula, ili wazidi kupotea, kuwa na shaka na kutokuwa na uamuzi, na Atawalipa kwa kuwacheza shere kwao Waislamu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net