Al-Baqara 2:14
البقرةوَإِذَا لَقُوا۟ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ قَالُوٓا۟ ءَامَنَّا وَإِذَا خَلَوْا۟ إِلَىٰ شَيَـٰطِينِهِمْ قَالُوٓا۟ إِنَّا مَعَكُمْ إِنَّمَا نَحْنُ مُسْتَهْزِءُونَ
Na wanapokutana na walioamini, husema: 'Tumeamini.' Na wanapokuwa peke yao na mashetani wao, husema: 'Hakika sisi tu pamoja nanyi. Hakika sisi tunafanya dhihaka tu.'
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wanapo kutana na walio amini husema: Tumeamini. Na wanapo kuwa peke yao na mashet'ani wao husema: Hakika sisi tu pamoja nanyi. Hakika sisi tunawadhihaki tu. [14]
[14] Hawa wanaafiki wakiwakuta Waumini wa kweli husema: "Sisi tunaamini hayo hayo mnayo amini nyinyi," yaani kumkubali Mtume na wito wake, "na sisi tu pamoja nanyi katika itikadi." Wakisha ondoka wakakutana na wenzao wanao shabihiana na mashetani kwa fitina na ufisadi, huwaambia: "Sisi tu pamoja nanyi katika njia yenu na kazi yenu, lakini tukiwaambia yale hao Waumini kwa ajili ya kuwalazia na kuwadhihaki tu."
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hawa wanafiki wakikutana na waumini huwa wakisema, “Tumeiamini Dini ya Uislamu kama nyinyi,” na wakiondoka kwenda kwa viongozi wao makafiri wasiomjali Allah Mtukufu, huwa wakiwahakikishia kuwa wao wako kwenye mila ya ukafiri, hawajaiacha, na kuwa wao walikuwa wakiwacheza shere waumini.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net