Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 13

Al-Baqara 2:13

البقرة

وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ ءَامِنُوا۟ كَمَآ ءَامَنَ ٱلنَّاسُ قَالُوٓا۟ أَنُؤْمِنُ كَمَآ ءَامَنَ ٱلسُّفَهَآءُ ۗ أَلَآ إِنَّهُمْ هُمُ ٱلسُّفَهَآءُ وَلَـٰكِن لَّا يَعْلَمُونَ

Maana

Na wanapoambiwa: Aminini kama walivyoamini watu. Husema: "Tuamini kama walivyoamini wapumbavu?" Hakika wao ndio wapumbavu, lakini hawajui tu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wanapo ambiwa: Aminini kama walivyo amini watu. Husema: Tuamini kama walivyo amini wapumbavu? Hakika wao ndio wapumbavu, lakini hawajui tu. [13]

[13] Akitokea mtu kuwanasihi na kuwaongoza kwa kuwaambia:"Kubalini yalio waajibu." Nako ni kuwa muamini Imani safi kama wanavyo amini watu wakamilifu wanao itikia wito wa akili, wao hufanya maskhara na kejeli na husema: "Si laiki yetu sisi kuwafuata hawa wajinga, wapungufu wa akili." Mwenyezi Mungu anawarudi kwa ule ubishi wao na kuwahukumia kuwa ni wao tu ndio wajinga, wapumbavu, lakini wao hawajui kwa ujuzi wa yakini kuwa ujinga na kukosa kuelewa ni kwao wao tu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na waambiwapo wanafiki, “Aminini kama walivyoamini masahaba, nako ni kuamini kwa moyo, ulimi na viungo,” huwa wakibisha na kusema, “Basi, tuamini kama vile madhaifu wa akili na maoni walivyoamini, tuwe kama wao katika upumbavu?” Allah Mtukufu aliwajibu kwamba udhaifu wa akili na maoni ni wao peke yao. Na wao hawajui kuwa msimamo walionao ndio upotevu na hasara.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net