Al-Baqara 2:16
البقرةأُو۟لَـٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ ٱشْتَرَوُا۟ ٱلضَّلَـٰلَةَ بِٱلْهُدَىٰ فَمَا رَبِحَت تِّجَـٰرَتُهُمْ وَمَا كَانُوا۟ مُهْتَدِينَ
Hao ndio walioununua upotovu kwa uongofu; lakini biashara yao haikupata faida, wala hawakuwa wenye kuongoka.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hao ndio walio nunua upotofu kwa uwongofu; lakini biashara yao haikupata tija, wala hawakuwa wenye kuongoka. [16]
[16] Na hawa (wanaafiki) kwa kukhiari upotofu badala ya uwongofu wamekuwa kama mfanya biashara aliye khiari kwa biashara yake bidhaa mbovu ya kuchina, basi hafanikiwi kupata faida yoyote. Hupoteza rasilmali yake. Na wao basi hawaongokewi katika 'amali yao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hao ndio wanafiki. Wamejiuza wenyewe katika mapatano ya hasara. Walichukuwa ukafiri na kuacha Imani. Hawakupata faida yoyote, bali walipata hasara ya kukosa uongofu. Huko ndiko kupata hasara kukubwa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net