Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 141

Al-Baqara 2:141

البقرة

تِلْكَ أُمَّةٌ قَدْ خَلَتْ ۖ لَهَا مَا كَسَبَتْ وَلَكُم مَّا كَسَبْتُمْ ۖ وَلَا تُسْـَٔلُونَ عَمَّا كَانُوا۟ يَعْمَلُونَ

Maana

Hao ni watu waliokwishapita. Wao watapata waliyoyachuma, na nyinyi mtapata mliyoyachuma, wala hamtaulizwa nyinyi yale waliyokuwa wakiyafanya wao.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hao ni watu walio kwisha pita. Wao watapata waliyo yachuma, na nyinyi mtapata mliyo yachuma, wala hamtaulizwa nyinyi yale waliyo kuwa wakifanya wao. [141]

[141] Tena imekuwaje nyinyi Mayahudi na Wakristo kuyajadili mambo ya watu hawa? Kwani watu hawa wamekwisha pita na njia zao. Wao watapata malipo ya a'mali yao waliyo itenda katika uhai wao, wala nyinyi hamtaulizwa juu ya a'mali zao, wala hamtafaidika kwa lolote katika hayo. Nanyi hamtapata malipo ila kwa vitendo mnavyo vifanya nyinyi wenyewe.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hao ni ummah waliopita miongoni mwa wale waliowatangulia nyinyi. Wao wana amali zao, na nyinyi muna amali zenu. Wala nyinyi hamtaulizwa kuhusu amali zao. Na wao hawataulizwa kuhusu amali zenu. Katika aya hii pana kukata njia ya kujifungamanisha na viumbe kwa kujiambatanisha nao, kutoghurika kwa kunasibiana na wao, kwa kuwa linalozingatiwa ni kumuamini Allah Mtukufu na kumuabudu Peke Yake na kuwafuata Mitume Wake, na kwamba mwenye kumkanusha Mtume yoyote katika wao, huwa amewakanusha Mitume wote.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net