Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 140

Al-Baqara 2:140

البقرة

أَمْ تَقُولُونَ إِنَّ إِبْرَٰهِـۧمَ وَإِسْمَـٰعِيلَ وَإِسْحَـٰقَ وَيَعْقُوبَ وَٱلْأَسْبَاطَ كَانُوا۟ هُودًا أَوْ نَصَـٰرَىٰ ۗ قُلْ ءَأَنتُمْ أَعْلَمُ أَمِ ٱللَّهُ ۗ وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّن كَتَمَ شَهَـٰدَةً عِندَهُۥ مِنَ ٱللَّهِ ۗ وَمَا ٱللَّهُ بِغَـٰفِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ

Maana

Au mnasema kuwa Ibrahim na Ismail na Is-hak na Yaakub na watoto wake walikuwa Mayahudi au Wakristo? Sema: Je, nyinyi mnajua zaidi au Mwenyezi Mungu? Na ni nani mwenye kudhulumu zaidi kuliko yule aliyeficha ushahidi alio nao utokao kwa Mwenyezi Mungu? Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika mbali na hayo myafanyayo.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Au mnasema kuwa Ibrahim na Ismail na Is-hak na Yaakub na wajukuu zao walikuwa Mayahudi au Wakristo? Sema: Je, nyinyi mnajua zaidi au Mwenyezi Mungu? Na ni nani mwenye kudhulumu zaidi kuliko yule aliye ficha ushahidi alio nao utokao kwa Mwenyezi Mungu? Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na hayo myafanyayo. [140]

[140] Waambieni: Mnajadiliana nasi katika mas-ala ya Ibrahim, na Ismail, na Is-hak, na Yaakub na watoto na wajukuu zao, mkidai kuwa wao walikuwa Mayahudi au Wakristo kama nyinyi, na ilhali Sisi hatukuiteremsha Taurati na Injili wanazo zitegemea Mayahudi na Wakristo ila baada ya hawa. Na Sisi tulikwisha waelezeni khabari ya hayo. Jee, nyinyi mnajua zaidi au Mwenyezi Mungu? Bali hakika Mwenyezi Mungu amekwisha waambieni nyinyi hayo katika vitabu vyenu. Basi msiifiche kweli iliyo andikwa katika hivi vitabu vyenu. Na nani dhaalimu mkubwa zaidi kuliko yule anaye ificha kweli inayo toka katika kitabu chake ambayo naye anaijua. Na Mwenyezi Mungu atakulipeni kwa upotovu mnao ushikilia, kwani Mwenyezi Mungu haghafiliki na mnayo yatenda.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Au je, Mnasema, kwa njia ya kujadili kuhusu Allah Mtukufu kwamba Ibrãhîm na Ismā‛īl na Is’ḥãq na Ya‛qûb na Asbãt – Manabii waliokuwa katika makabila kumi na mbili ya Wana wa Isrãîl wanaotokana na wana wa Ya‛qûb – walikuwa katika dini ya Kiyahudi au ya Kinaswara? Huu ni urongo. Kwani hao walitumilizwa na kufa kabla ya Taurati na Injili. Waambie, ewe Mtume, “Kwani ni nyinyi mnaoijua zaidi dini yao au ni Allah Mtukufu?” Na Allah Mtukufu Ameshaeleza katika Qur’ani kwamba wao walikuwa Waislamu wenye msimamo uliolingana sawa. Na hakuna yoyote dhalimu zaidi kuliko nyinyi mnapouficha ushahidi uliothibiti kwenu kutoka kwa Allah Mtukufu na kudai kinyume chake kwa kumzulia Allah Mtukufu urongo. Na Allah Mtukufu si Mwenye kughafilika na chochote katika vitendo vyenu. Yeye ni Mwenye kuvidhibiti na ni Mwenye kuwalipa kwavyo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net