Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 131

Al-Baqara 2:131

البقرة

إِذْ قَالَ لَهُۥ رَبُّهُۥٓ أَسْلِمْ ۖ قَالَ أَسْلَمْتُ لِرَبِّ ٱلْعَـٰلَمِينَ

Maana

Na Mola wake Mlezi alipomwambia: Silimu! Akasema: Nimesilimu kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na Mola wake Mlezi alipo mwambia: Silimu, Nyenyekea! Alinena: Nimesilimu, nimenyenyekea kwa Mola wa walimwengu wote. [131]

[131] Yeye Ibrahim aliitikia amri ya Mola wake Mlezi pale alipo mtaka asilimu, yaani anyenyekee. Akasema: Namnyenyekea Mola Mlezi wa walimwengu wote, majini, watu na Malaika.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na sababu ya kuchaguliwa kwake huku ni kukimbilia kwake kwenye Uislamu bila kusita. Alipoambiwa na Mola wake, “Itakase nafsi yako kwa Allah Mtukufu kwa kujisalimisha Kwake” alikubali Ibrãhîm na kusema, “Nimejisalimisha kwa Mola wa viumbe vyote, kwa kumtakasa, kumpwekesha, kumpenda na kurudi Kwake kwa kutubia.”

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net