Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 132

Al-Baqara 2:132

البقرة

وَوَصَّىٰ بِهَآ إِبْرَٰهِـۧمُ بَنِيهِ وَيَعْقُوبُ يَـٰبَنِىَّ إِنَّ ٱللَّهَ ٱصْطَفَىٰ لَكُمُ ٱلدِّينَ فَلَا تَمُوتُنَّ إِلَّا وَأَنتُم مُّسْلِمُونَ

Maana

Na Ibrahim akawausia wanawe hilo, na pia Yaaqub: Enyi wanangu! Hakika Mwenyezi Mungu amekuteulieni Dini hii. Basi kamwe msife ila nanyi ni Waislamu.[1]

[1] Yani aliichagua na akawateulia kama rehema na wema. Basi inapasa kusimama nayo na kusifika kwa sheria zake, na kujipaka maadili yake na kudumu namna hiyo hadi kifo. Kwa sababu, mwenye kuishi juu ya kitu, atakufa juu yake. Na mwenye kufa juu ya kitu, atafufuliwa juu yake.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na Ibrahim akawausia wanawe, na pia Yaaqub: Enyi wanangu! Hakika Mwenyezi Mungu amekuteulieni Dini hii; basi msife ila nanyi mmekuwa Waislamu, wanyenyekevu. [132]

[132] Na Ibrahim hakutosheka na hayo tu, bali aliwausia wanawe wende mwendo wa uwongofu kama wake. Na mjukuu wake Yaakubu akamuiga, naye akawausia wanawe kadhaalika wafuate mwenendo huo huo. Aliwabainishia wanawe ya kwamba Mwenyezi Mungu amewateulia Dini ya Tawhidi, ya Mungu Mmoja. Na akachukua kwao ahadi kuwa hawatakufa ila nao ni Waislamu, wenye kuthibiti juu ya Dini hii.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na Ibrãhîm na Ya‛qûb waliwahimiza watoto wao kusimama imara juu ya Uislamu wakiwaambia, “Enyi watoto wetu! Allah Mtukufu Amewachagulia Dini hii, nayo ni Uislamu, Msiiache muda wa uhai wenu, na msifikiwe na mauti isipokuwa na nyinyi muko kwenye Dini hii.”

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net