Al-Baqara 2:130
البقرةوَمَن يَرْغَبُ عَن مِّلَّةِ إِبْرَٰهِـۧمَ إِلَّا مَن سَفِهَ نَفْسَهُۥ ۚ وَلَقَدِ ٱصْطَفَيْنَـٰهُ فِى ٱلدُّنْيَا ۖ وَإِنَّهُۥ فِى ٱلْـَٔاخِرَةِ لَمِنَ ٱلصَّـٰلِحِينَ
Na nani atajitenga na mila ya Ibrahim isipokuwa anayeitia nafsi yake katika upumbavu? Na kwa yakini, Sisi tulimteua yeye katika dunia. Na hakika yeye katika Akhera atakuwa miongoni mwa watu wema.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na nani atajitenga na mila ya Ibrahim isipo kuwa anayeitia nafsi yake katika upumbavu? Na kwa yakini Sisi tulimteuwa yeye katika dunia; na hakika yeye katika Akhera atakuwa miongoni mwa watu wema. [130]
[130] Aliyo yafanya Ibrahim na aliyo yaomba kwa Mwenyezi Mungu ni mambo mazuri mno. Hali kadhaalika mila aliyo ifuata ni mila iliyo kwenda sawa kabisa. Na hapana anaye jitenga na mila ya Ibrahim ila mwenye kuudharau utu wake mwenyewe na akili yake. Hakika Mwenyezi Mungu alimteuwa yeye Ibrahim katika dunia, na pia Akhera ni miongoni mwa watu wema walio karibishwa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakuna yoyote anayeipa mgongo Dini ya Ibrãhîm, nayo ni Uislamu, isipokuwa safihi aliye mjinga. Na hakika tulimchagua Ibrãhîm duniani kuwa Nabii na Mtume, na kesho Akhera kuwa ni miongoni mwa watu wema ambao wana daraja za juu kabisa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net