Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Baqara
Sura ya 2

Al-Baqara

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya ya 130

وَمَن يَرْغَبُ عَن مِّلَّةِ إِبْرَٰهِـۧمَ إِلَّا مَن سَفِهَ نَفْسَهُۥ ۚ وَلَقَدِ ٱصْطَفَيْنَـٰهُ فِى ٱلدُّنْيَا ۖ وَإِنَّهُۥ فِى ٱلْـَٔاخِرَةِ لَمِنَ ٱلصَّـٰلِحِينَ 130

Na Ibrahim alipomtukuza Mwenyezi Mungu, huku kumtukuza, na akaeleza sifa zake kamilifu, Yeye Mtukufu akasema:

(130) Yani hajitengi "na mila ya Ibrahim" baada ya kujua katika fadhila zake, "isipokuwa anayeitia nafsi yake katika upumbavu?" Yani aliipuuza, akaidhalilisha, akaikubalia kuwa duni, na akaiuza kwa mapatano ya waliopunjwa. Kama vile hakuna mwongofu na mkamilifu zaidi kuliko mwenye kuitaka mila ya Ibrahim. Kisha akaeleza kuhusu hali yake katika dunia na Akhera, akasema: "Na kwa yakini, Sisi tulimteua yeye katika dunia." Yani tulimchagua na tukamwezesha kufanya matendo ambayo kwayo aliweza kuwa miongoni mwa wateule walio bora. "Na hakika yeye katika Akhera atakuwa miongoni mwa watu wema." ambao wana daraja za juu zaidi.