Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 112

Al-Baqara 2:112

البقرة

بَلَىٰ مَنْ أَسْلَمَ وَجْهَهُۥ لِلَّهِ وَهُوَ مُحْسِنٌ فَلَهُۥٓ أَجْرُهُۥ عِندَ رَبِّهِۦ وَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ

Maana

Sivyo hivyo! Yeyote anayeelekeza uso wake kwa Mwenyezi Mungu, naye ni mtenda mema, basi ana malipo yake kwa Mola wake Mlezi; wala haitakuwa hofu juu yao wala hawatahuzunika.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Sivyo hivyo! Yeyote anaye elekeza uso wake kwa Mwenyezi Mungu naye ni mtenda mema, basi ana malipo yake kwa Mola wake Mlezi, wala haitakuwa khofu juu yao wala hawatahuzunika. [112]

[112] Na wala hawatapata ushahidi wa hilo. Kwani kweli ilivyo ni kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu amewaandalia neema za Pepo, na atawalipa malipo Siku ya Kiyama, na atawalinda na khofu na huzuni, hao ambao wanao msafia niya Mwenyezi Mungu na wanafuata Haki, na vitendo wavitendavyo ni vyema.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Mambo si kama walivyodhania kuwa Pepo ni ya pote fulani tu, si ya pote lingine. Hakika ataingia Peponi mwenye kumtakasa Allah Mtukufu Peke Yake Asiye na mshirika na akawa ni mwenye kumfuata Mtume Muhammad, rehema na amani zimshukie, katika maneno yake yote na vitendo vyake vyote. Basi mwenye kufanya hayo atakuwa na thawabu ya matendo yake mbele ya Mola wake huko Akhera, nayo ni kuingia Peponi, hali ya kuwa wao, hao wenye kuingia Peponi, hawaogopi mambo ya Akhera yanayowakabili mbele yao, wala hawahuzuniki juu ya hadhi za ulimwengu zilizowapita.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net