Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Baqara
Sura ya 2

Al-Baqara

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya ya 112

بَلَىٰ مَنْ أَسْلَمَ وَجْهَهُۥ لِلَّهِ وَهُوَ مُحْسِنٌ فَلَهُۥٓ أَجْرُهُۥ عِندَ رَبِّهِۦ وَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ 112

(112) Kisha Mwenyezi Mungu akataja dalili zilizo wazi, zenye kujumuisha kila mtu, akasema: "Sivyo hivyo!" yani sio kwa matamanio yenu wala madai yenu. Lakini "yeyote anayeelekeza uso wake kwa Mwenyezi Mungu;" yani anayemfanyia Mwenyezi Mungu peke yake matendo yake, huku amemwelekea kwa moyo wake "naye ni mtenda mema" katika kumwabudu Mola wake Mlezi, kwa kumwabudu kwa sheria yake, basi hao ndio watu wa Peponi peke yao. Nao wana malipo yao kwa Mola wao Mlezi. Nayo ni Pepo iliyomo pamoja na ilivyojumuisha ndani yake miongoni mwa neema "wala haitakuwa hofu juu yao wala hawatahuzunika." Basi wakapata yanayotamaniwa, na wakaokoka kutokana na yanayohofisha. Na inafahamika kutoka humo kwamba asiyekuwa hivyo, basi huyo ni katika watu wa Motoni walioangamia. Hivyo, hakuna wokovu wowote ila kwa watu wenye ikhlasi (wanomfanyia matendo Mwenyezi Mungu peke yake) kwa mwabudiwa wao na kumfuata Mtume (wa Mwenyezi Mungu).