Al-Baqara 2:113
البقرةوَقَالَتِ ٱلْيَهُودُ لَيْسَتِ ٱلنَّصَـٰرَىٰ عَلَىٰ شَىْءٍ وَقَالَتِ ٱلنَّصَـٰرَىٰ لَيْسَتِ ٱلْيَهُودُ عَلَىٰ شَىْءٍ وَهُمْ يَتْلُونَ ٱلْكِتَـٰبَ ۗ كَذَٰلِكَ قَالَ ٱلَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ مِثْلَ قَوْلِهِمْ ۚ فَٱللَّهُ يَحْكُمُ بَيْنَهُمْ يَوْمَ ٱلْقِيَـٰمَةِ فِيمَا كَانُوا۟ فِيهِ يَخْتَلِفُونَ
Na Mayahudi husema: Wakristo hawana lao jambo (wanalolifuata). Na Wakristo husema: Mayahudi hawana lao jambo (wanalolifuata). Na ilhali wote wanasoma Kitabu kicho hicho (Biblia). Na kadhaalika walisema wale wasiojua kitu mfano wa kauli yao hii. Basi Mwenyezi Mungu atahukumu baina yao Siku ya Kiyama katika yale waliyokuwa wakihitilafiana.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na Mayahudi husema: Wakristo hawana lao jambo. Na Wakristo husema: Mayahudi hawana lao jambo. Na ilhali wote wanasoma Kitabu hicho hicho (Biblia). Na kadhaalika walisema wale wasio jua kitu mfano wa kauli yao hii. Basi Mwenyezi Mungu atahukumu baina yao Siku ya Kiyama katika yale waliyo kuwa wakikhitilafiana. [113]
[113] Na ajabu iliyopo ni kuwa kama wanavyo fanyia uadui Uislamu, wanafanyiana uadui wenyewe, wao kwa wao. Mayahudi husema: Wakristo hawana lolote la haki. Na Wakristo nao wanasema mfano wa hayo, na huku wote wawili wanatoa ushahidi wao kutoka hivyo hivyo vitabu vyao vya Biblia wanavyoviamini wao wote. Na wale washirikina wa Kiarabu wasio jua chochote katika vitabu vilivyo teremshwa kwa Mayahudi na Wakristo husema maneno kama hayo. Na kwa hakika wote hao pamoja wamesema kweli, kwani hapana kikundi kimojapo katika wao kilicho kuwamo katika Haki. Na hayo yatabainika pale Mwenyezi Mungu atapo wahukumu Siku ya Kiyama katika zile khitilafu zao wanazo khitilafiana.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na walisema Mayahudi, “Wanaswara hawako kwenye dini sahihi. Ndivyo hivyo kama walivyosema Wanaswara kuhusu Mayahudi, na hali wote wanasoma Taurati na Injili, ambapo ndani yake kuna ulazima wa kuwaamini Mitume wote. Hivyo ndivyo pia walivyosema wasiojua miongoni mwa washirikina: Waarabu na wengineo. Yaani, walisema kumwambia kila mwenye dini, “Wewe huko kwenye kitu chochote cha maana.” Basi Allah Mtukufu Ataamua baina yao Siku ya Kiyama katika yale mambo ya kidini waliotafautiana juu yake, na kumlipa kila mtu kwa matendo yake aliyoyafanya.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net