Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 107

Al-Baqara 2:107

البقرة

أَلَمْ تَعْلَمْ أَنَّ ٱللَّهَ لَهُۥ مُلْكُ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ ۗ وَمَا لَكُم مِّن دُونِ ٱللَّهِ مِن وَلِىٍّ وَلَا نَصِيرٍ

Maana

Je, hujui kwamba Mwenyezi Mungu ana ufalme wa Mbingu na Ardhi? Nanyi hamna mlinzi wala msaidizi isipokuwa Mwenyezi Mungu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hujui kwamba Mwenyezi Mungu ana ufalme wa Mbingu na Ardhi? Nanyi hamna mlinzi wala msaidizi isipo kuwa Mwenyezi Mungu. [107]

[107] Na Yeye, Mwenyezi Mungu, ndiye mwenye ufalme wa Mbingu na Ardhi katika mikono yake. Na nyinyi watu hamna mlinzi wa kukusaidieni, wala tegemeo la kukunusuruni isipokuwa Yeye.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kwani hukujua, ewe Nabii, wewe na ummah wako, kwamba Allah Mtukufu Ndiye Mwenye kumiliki, Ndiye Mwenye kuendesha mambo ya mbinguni na ardhini? Anafanya Analolitaka na Anatoa uamuzi Anaotaka. Anawaamrisha waja Wake na kuwakataza Anavyotaka, na ni juu yao kutii na kukubali. Na wajue wenye kumuasi Yeye kuwa hakuna rafiki mwenye kuwasaidia wala muokozi mwenye kuzuia adhabu ya Allah Mtukufu isiwapate.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net