Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 108

Al-Baqara 2:108

البقرة

أَمْ تُرِيدُونَ أَن تَسْـَٔلُوا۟ رَسُولَكُمْ كَمَا سُئِلَ مُوسَىٰ مِن قَبْلُ ۗ وَمَن يَتَبَدَّلِ ٱلْكُفْرَ بِٱلْإِيمَـٰنِ فَقَدْ ضَلَّ سَوَآءَ ٱلسَّبِيلِ

Maana

Au mnataka kumuuliza Mtume wenu kama alivyoulizwa Musa zamani? Na anayebadilisha Imani kwa ukafiri, bila ya shaka, huyo ameipotea njia iliyo sawa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Au mnataka kumwomba Mtume wenu kama alivyo ombwa Musa zamani? Na anaye badilisha Imani kwa ukafiri bila ya shaka huyo ameipotea njia iliyo sawa. [108]

[108] Na kwa kule kumtaka kwenu Mtume wenu Muhammad miujiza fulani pengine ilikuwa mnawaiga Wana wa Israili wa zama za Musa, walipo mtaka awaletee miujiza maalumu. Kutaka kwenu huku kunaficha nyuma yake inda na kumili kwenye ukafiri, kama kulivyo kuwa kule kutaka kwa Wana wa Israili kumtaka Mtume wao. Na mwenye kufuata nyayo za inda na ukafiri akaacha usafi wa kutaka Haki na Imani basi huyo ameipotea Njia iliyo sawa iliyo nyooka.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Bali nyinyi mnataka, enyi watu, kumuuliza Mtume wenu Muhammad, rehema na amani zimshukie, awapatie mambo, kwa njia ya ukaidi na ujeuri, kama yalivyotakwa, mfano wa hayo, kutoka kwa Mûsã. Na jueni kwamba mwenye kuchagua ukafiri na kuacha Imani, ashatoka nje ya njia ya Allah Mtukufu iliyolingana sawa na ameingia kwenye ujinga na upotevu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net