Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Baqara
Sura ya 2

Al-Baqara

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya ya 107

أَلَمْ تَعْلَمْ أَنَّ ٱللَّهَ لَهُۥ مُلْكُ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ ۗ وَمَا لَكُم مِّن دُونِ ٱللَّهِ مِن وَلِىٍّ وَلَا نَصِيرٍ 107

(107) "Je, hujui kwamba Mwenyezi Mungu ana ufalme wa Mbingu na Ardhi?" Basi ikiwa yeye ni mmiliki wenu, anayewaendesha kuendesha kwa mmiliki mwema, mwenye huruma katika makadirio yake, na maamrisho yake, na makatazo yake. Na kama vile hakuna kizuizi chochote juu yake katika kukadiria anayoyakadiria juu ya waja wake miongoni mwa aina za makadirio, basi kadhalika asimpinge katika yale anayowawekea waja wake miongoni mwa hukumu. Hivyo basi, mja anatawaliwa, amefanywa kuwa chini ya amri za kidini na za kimakadirio za Mola wake Mlezi. Vipi sasa atapinga? Naye pia ni mlinzi wa waja wake na msaidizi wao. Anawachunga katika kupata manufaa yao, na anawasaidia katika kuwaondolea madhara yao. Na katika kuwachunga ni kwamba awaekee hukumu kulingana na inavyohitajiwa na hekima yake na rehema yake kwao. Na anayetafakari yaliyotokea katika Qur-ani na Sunna ya ufutaji, atajua kwa hilo, hekima ya Mwenyezi Mungu na rehema yake kwa waja wake. Na kuwafikisha kwenye masilahi yao kutoka pale wasipotambua kwa sababu ya upole wake.