Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 103

Al-Baqara 2:103

البقرة

وَلَوْ أَنَّهُمْ ءَامَنُوا۟ وَٱتَّقَوْا۟ لَمَثُوبَةٌ مِّنْ عِندِ ٱللَّهِ خَيْرٌ ۖ لَّوْ كَانُوا۟ يَعْلَمُونَ

Maana

Na lau kuwa wangeamini na wakamcha Mungu, bila ya shaka malipo yatokayo kwa Mwenyezi Mungu yangekuwa bora. Laiti wangelikuwa wanajua!

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na lau kuwa wangeamini na wakaogopa, bila ya shaka malipo yatokayo kwa Mwenyezi Mungu yange kuwa bora. Laiti wangeli kuwa wanajua! [103]

[103] Na lau kuwa wao wameiamini Haki na wakauogopa ufalme na uwezo wa Mola wao Mlezi, basi Mwenyezi Mungu angeli walipa malipo mema, na hayo bila ya shaka yoyote yangeli kuwa ni bora zaidi kuliko wanayo yapata katika hadithi zao za uwongo na dhamiri zao mbovu wanazo zidhamiria, lau kuwa wanabagua linalo kuwa na manufaa wakaacha lenye madhara.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na lau Mayahudi wangeamini na kumuogopa Allah Mtukufu, wangalikuwa na yakini kuwa thawabu za Allah Mtukufu ni bora kwao kuliko uchawi na kuliko yale waliyoyapata kupitia huo uchawi. Lau wangekua wanajua thawabu na malipo yanayopatikana kwa kuamini na kumcha Allah Mtukufu, ujuzi wa kihakika, wangaliamini.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net