Al-Baqara 2:10
البقرةفِى قُلُوبِهِم مَّرَضٌ فَزَادَهُمُ ٱللَّهُ مَرَضًا ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌۢ بِمَا كَانُوا۟ يَكْذِبُونَ
Nyoyoni mwao kuna maradhi[1], na Mwenyezi Mungu amewazidishia maradhi. Basi watakuwa na adhabu chungu kwa sababu ya kusema kwao uongo.
[1] Kilichokusudiwa na maradhi hapa ni maradhi ya shaka, dhana potovu na unafiki.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Nyoyoni mwao mna maradhi, na Mwenyezi Mungu amewazidishia maradhi. Basi watakuwa na adhabu chungu kwa sababu ya kusema kwao uwongo. [10]
[10] Katika nyoyo za watu hawa mna maradhi ya uhasidi na chuki kwa watu wenye imini, na itikadi zao zimefisidika. Mwenyezi Mungu basi anawazidishia hayo maradhi yao, kwa ajili ya kuinusuru Haki, kwani hayo yanawaudhi wao kwa sababu ya uhasidi wao, na chuki yao, na inadi yao. Watu hao watapata adhabu iliyo chungu Duniani na Akhera kwa sababu ya uwongo wao na upinzani wao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Ndani ya nyoyo zao kuna shaka na uharibifu, ndipo wakaonjwa kwa kufanya maasia yenye kuwafanya wastahiki kuadhibiwa, na Allah Mtukufu akawazidishia shaka. Watakuwa na adhabu yenye uchungu kwa sababu ya urongo na unafiki wao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net