Al-Baqara 2:11
البقرةوَإِذَا قِيلَ لَهُمْ لَا تُفْسِدُوا۟ فِى ٱلْأَرْضِ قَالُوٓا۟ إِنَّمَا نَحْنُ مُصْلِحُونَ
Na wanapoambiwa: Msifanye uharibifu katika ardhi. Husema: "Bali sisi ni watengenezaji."
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wanapo ambiwa: Msifanye uharibifu ulimwenguni. Husema: Bali sisi ni watengenezaji. [11]
[11] Na pindi mmojawapo wa walio ongoka akiwaambia hawa wanaafiki: "Msifanye uharibifu katika nchi kwa kuipinga Njia ya Mwenyezi Mungu, na kueneza fitna, na kuwasha moto wa vita," wao hujitoa makosani mwa uharibifu, na husema: "Kee sisi ndio tunao tengeneza." Na hayo ni kwa kuwa ghururi yao imepita mpaka. Huu ndio mwendo wa kila mharibifu, khabithi mwenye ghururi. Yeye hudai kuwa ule uharibifu wake ndio matengenezo na maendeleo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wanapopewa nasaha wakome kufanya uharibifu katika ardhi kwa kukanusha na kuasi kutoa siri za Waumini na kuwategemea makafiri, wanasema kwa urongo na kubisha, “Sisi ndio watu wakutengeneza.”
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net