Maryam 19:58
مريمأُو۟لَـٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ أَنْعَمَ ٱللَّهُ عَلَيْهِم مِّنَ ٱلنَّبِيِّـۧنَ مِن ذُرِّيَّةِ ءَادَمَ وَمِمَّنْ حَمَلْنَا مَعَ نُوحٍ وَمِن ذُرِّيَّةِ إِبْرَٰهِيمَ وَإِسْرَٰٓءِيلَ وَمِمَّنْ هَدَيْنَا وَٱجْتَبَيْنَآ ۚ إِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ ءَايَـٰتُ ٱلرَّحْمَـٰنِ خَرُّوا۟ سُجَّدًا وَبُكِيًّا ۩
Hao ndio aliowaneemesha Mwenyezi Mungu miongoni mwa Manabii katika uzao wa Adam, na katika uzao wa wale tuliowabeba pamoja na Nuhu, na katika uzao wa Ibrahim na Israili, na katika wale tuliowaongoa na tukawateua. Wanaposomewa Aya za Mwingi wa rehema, huanguka kusujudu na kulia.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hao ndio alio waneemesha Mwenyezi Mungu miongoni mwa Manabii katika uzao wa Adam, na katika uzao wa wale tulio wapandisha pamoja na Nuhu, na katika uzao wa Ibrahim na Israil, na katika wale tulio waongoa na tukawateuwa. Wanapo somewa Aya za Mwingi wa Rehema huanguka kusujudu na kulia.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hawa niliokusimulia habari zao, ewe Mtume, ni wale ambao Allah Mtukufu Amewaneemesha kwa nyongeza Zake na taufiki Yake, Akawafanya ni Mitume miongoni mwa kizazi cha Ãdam, na miongoni mwa kizazi cha wale tuliowabeba pamoja na Nûh, katika jahazi, na miongoni mwa kizazi cha Ibrãhîm, na miongoni mwa kizazi cha Ya‛qûb, na miongoni mwa wale tuliowaongoza kwenye Imani na tukawateua kwa utume na unabii. Wasomewapo aya za Mwingi wa rehema zinazokusanya upweke Wake na hoja Zake wanajiporomosha chini hali ya kumsujudia Allah Mtukufu kwa kunyenyekea na kujidhalilisha, na wanalia kwa kumcha Yeye, kutakasika ni Kwake na kutukuka ni Kwake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net