Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 19 · Aya ya 59

Maryam 19:59

مريم

فَخَلَفَ مِنۢ بَعْدِهِمْ خَلْفٌ أَضَاعُوا۟ ٱلصَّلَوٰةَ وَٱتَّبَعُوا۟ ٱلشَّهَوَٰتِ ۖ فَسَوْفَ يَلْقَوْنَ غَيًّا

Maana

Lakini wakaja baada yao wafuatizi walioipoteza Swala, na wakafuata matamanio. Basi watakujakuta malipo ya ubaya.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Lakini wakaja baada yao walio wabaya, wakaacha Swala, na wakafuata matamanio. Basi watakuja kuta malipo ya ubaya.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wakaja, baada ya hawa walioneemeshwa, wafuasi wabaya, ambao waliacha Swala kabisa au waliitoa nje ya wakati wake, au waliacha nguzo zake na mambo yake ya lazima na wakafuata yanayolingana na kunasibiana na matamanio yao. Basi hao watapata shari na upotevu na kuhuzunika ndani ya Jahanamu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Maryam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net