Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 18 · Aya ya 97

Al-Kahf 18:97

الكهف

فَمَا ٱسْطَـٰعُوٓا۟ أَن يَظْهَرُوهُ وَمَا ٱسْتَطَـٰعُوا۟ لَهُۥ نَقْبًا

Maana

Basi hawakuweza kukikwea, wala hawakuweza kukitoboa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi hawakuweza kuukwea, wala hawakuweza kuutoboa. [97]

[97] Basi wale mahasidi hawakuweza kulikwea lile boma, jinsi lilivyo kwenda juu, wala kulitoboa kwa ugumu wake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hawakuweza Ya’jûj na Ma’jûj kupanda juu ya kile kizuizi kwa kuwa kilikuwa kirefu na kinateleza, na hawakuweza kukitoboa kwa chini yake kwa umbali wa upana wake na ugumu wake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Kahf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net