Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 18 · Aya ya 98

Al-Kahf 18:98

الكهف

قَالَ هَـٰذَا رَحْمَةٌ مِّن رَّبِّى ۖ فَإِذَا جَآءَ وَعْدُ رَبِّى جَعَلَهُۥ دَكَّآءَ ۖ وَكَانَ وَعْدُ رَبِّى حَقًّا

Maana

Akasema, "Hii ni rehema kutoka kwa Mola wangu Mlezi. Na itakapokuja ahadi ya Mola wangu Mlezi, atakivunjavunja. Na ahadi ya Mola wangu Mlezi ni ya kweli."

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Akasema: Hii ni rehema itokayo kwa Mola wangu Mlezi. Na itapo fika ahadi ya Mola wangu Mlezi atauvunja vunja. Na ahadi ya Mola wangu Mlezi ni kweli tu. [98]

[98] Dhul-Qarnaini alipo kwisha jenga ile ngome alisema kumshukuru Mwenyezi Mungu: Ngome hii ni rehema iliyo toka kwa Mola wangu Mlezi kwa ajili ya waja wake. Na itabaki hivi hivi imesimama mpaka ije amri ya Mwenyezi Mungu kuiteketeza. Hapo tena itakuwa sawa sawa na ardhi. Na amri ya Mwenyezi Mungu ni lazima itimie bila ya muhali.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Dhulqarnain akasema, «Hiki nilichokijenga cha kuzuia uharibifu wa Ya’jûj na Ma’jûj ni rehema kwa watu itokayo kwa Mola wangu, na ahadi ya Allah Mtukufu itakapokuja ya kutoka Ya’jûj na Ma’jûj, Atakifanya kigongeke gongeke kivunjike na kiwe sawa na ardhi, na ahadi ya Allah Mtukufu ni ya kweli».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Kahf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net