Al-Kahf 18:96
الكهفءَاتُونِى زُبَرَ ٱلْحَدِيدِ ۖ حَتَّىٰٓ إِذَا سَاوَىٰ بَيْنَ ٱلصَّدَفَيْنِ قَالَ ٱنفُخُوا۟ ۖ حَتَّىٰٓ إِذَا جَعَلَهُۥ نَارًا قَالَ ءَاتُونِىٓ أُفْرِغْ عَلَيْهِ قِطْرًا
Nileteeni vipande vya chuma. Hata alipoijaza sawasawa nafasi iliyo katikati ya milima miwili hiyo, akasema, "Pulizeni moto" mpaka alipokifanya kuwa moto, akasema, "Nileteeni shaba iliyoyeyuka niimimine juu ya chuma hicho."
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Nileteeni vipande vya chuma. Hata alipo ijaza nafasi iliyo kati ya milima miwili, akasema: Vukuteni. Hata alipo kifanya (chuma) kama moto akasema: Nileteeni shaba iliyo yayuka niimwagie. [96]
[96] Akawataka wamkusanyie vipande vya chuma. Wakakusanya kama alivyo taka. Akajenga kwa hivyo ngome ndefu iliyo lingana na kingo za milima hiyo miwili. Kisha akawaamrisha wawashe moto, wakauwasha, mpaka chuma kikayayuka. Tena akamimina juu yake shaba iliyo kwisha yayushwa; ikawa ngome madhubuti, haipitiki.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
«Nipeni vipande vya chuma» Walipokuja navyo, wakaviweka na wakavipanga karibu baina ya yale majabali mawili, aliwaambia wanaofanya kazi, «Washeni moto.» Na kilipogeuka chuma kuwa moto alisema, «Nipatieni shaba iliyoyayuka niimimine juu yake».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net