Al-Kahf 18:79
الكهفأَمَّا ٱلسَّفِينَةُ فَكَانَتْ لِمَسَـٰكِينَ يَعْمَلُونَ فِى ٱلْبَحْرِ فَأَرَدتُّ أَنْ أَعِيبَهَا وَكَانَ وَرَآءَهُم مَّلِكٌ يَأْخُذُ كُلَّ سَفِينَةٍ غَصْبًا
Ama lile jahazi, hilo lilikuwa la masikini fulani wafanyao kazi baharini. Kwa hivyo, nilitaka kulitia dosari, kwani nyuma yao alikuwapo mfalme aliyekuwa akichukua kwa nguvu majahazi yote.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Ama ile jahazi ilikuwa ya masikini za Mungu wafanyao kazi baharini. Nilitaka kuiharibu, kwani nyuma yao alikuwako mfalme anaghusubu majahazi yote. [79]
[79] Ama ile jahazi niliyo itoboa ilikuwa ni ya watu wanyonge wenye haja, ambao kazi yao ni ya baharini wakitafuta riziki yao. Basi mimi nikataka kukitia ila chombo chao kisitakikane. Kwani nyuma yao yuko mfalme mtindo wake ni kupokonya kila jahazi nzima. (Kughusubu, kupokonya, hata kukiitwa "kutaifisha" ni dhambi kubwa kabisa kwa Mwenyezi Mungu, kwani ni dhulma.)
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Ama mashua ambayo niliitoboa tundu, ilikuwa ni ya watu masikini wanaofanya kazi baharini wakiwa ndani yake wakijitafutia riziki, nikataka kuitia dowa kwa kuitoboa, kwa kuwa mbele yao kulikuwa na mfalme anayechukua kila mashua nzuri kwa kuwanyang’anya wenyewe.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net