Al-Kahf 18:78
الكهفقَالَ هَـٰذَا فِرَاقُ بَيْنِى وَبَيْنِكَ ۚ سَأُنَبِّئُكَ بِتَأْوِيلِ مَا لَمْ تَسْتَطِع عَّلَيْهِ صَبْرًا
(Yule mtu) akasema: Huku ndiko kutengana baina yangu na wewe. Sasa nitakueleza maana ya yale ambayo hukuweza kuyastahamili.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
(Yule mtu) akasema: Huku ndio kufarikiana baina yangu na wewe. Sasa nitakueleza maana ya yale uliyo kuwa huwezi kuyastahamilia. [78]
[78] Mja mwema akasema: Huku kutaaradhi kwako mara kwa mara kwa niyatendayo mimi ndio sababu ya kufarikiana mimi nawe. Sasa basi nitakueleza hikima ya yote haya ambayo wewe huyajui undani wake, wala hukuweza kuyasubiria yaliyo fichikana ukangojea kujua hakika yake na siri yake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Al-Khiḍr akamwambia Mûsã, Huu ndio wakati wa kutengana mimi na wewe. Nitakuelezea habari ya matendo yangu niliyoyafanya ambayo wewe ulinipinga nayo na ambayo hukuweza kuwa na uvumilivu wa kutoyauliza na kutonipinga mimi kuhusu hayo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net