Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 18 · Aya ya 77

Al-Kahf 18:77

الكهف

فَٱنطَلَقَا حَتَّىٰٓ إِذَآ أَتَيَآ أَهْلَ قَرْيَةٍ ٱسْتَطْعَمَآ أَهْلَهَا فَأَبَوْا۟ أَن يُضَيِّفُوهُمَا فَوَجَدَا فِيهَا جِدَارًا يُرِيدُ أَن يَنقَضَّ فَأَقَامَهُۥ ۖ قَالَ لَوْ شِئْتَ لَتَّخَذْتَ عَلَيْهِ أَجْرًا

Maana

Basi wakaondoka mpaka wakawafikia watu wa mji mmoja. Wakawaomba watu wake wawape chakula, nao wakakataa kuwakaribisha. Hapo wakakuta ukuta unataka kuanguka, (yule mja mwema) akausimamisha. (Musa) akasema, "Ungelitaka, ungelichukua ujira kwa haya."

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi wakatoka mpaka wakawafikia watu wa mji mmoja. Wakawaomba watu wake wawape chakula, nao wakakataa kuwakaribisha. Hapo wakakuta ukuta unataka kuanguka, (yule mja mwema) akausimamisha. (Musa) akasema: Ungeli taka ungeli chukua ujira kwa haya. [77]

[77] Wakenda hata wakafika kwenye mji. Wakawataka watu wake wawape chakula, wakakataa kuwakirimu. Wakakuta ukuta umeinama wakaribia kuanguka. Yule mja mwema akaudiriki. Akaujenga mpaka akausimamisha sawa. Musa akasema: Ungeli taka ungeli weza kudai ujira kwa kazi uliyo ifanya.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Mûsã akaenda na Al-Khiḍr mpaka wakafika kwa watu wa kijiji, wakataka wapewe chakula kwa njia ya makaribisho. Watu wa kijijini walikataa kuwakaribisha. Kisha wao wawili walipata hapo ukuta ulioinama uliokaribia kuanguka, Al- Khiḍr akautengeneza mpaka ukawa uko sawa. Mûsã akamwambia, «Lau ungalitaka ungalichukua kwa kazi hii malipo ukayatumia kujipatia chakula chetu kwa kuwa wao hawakutukaribisha».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Kahf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net