Al-Kahf 18:80
الكهفوَأَمَّا ٱلْغُلَـٰمُ فَكَانَ أَبَوَاهُ مُؤْمِنَيْنِ فَخَشِينَآ أَن يُرْهِقَهُمَا طُغْيَـٰنًا وَكُفْرًا
Na ama yule kijana, wazazi wake walikuwa ni Waumini. Tukahofu aje kuwatia mashakani kwa kupindukia mipaka na ukafiri.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na ama yule kijana, wazazi wake walikuwa ni Waumini. Tukakhofu asije watia mashakani kwa uasi na ukafiri. [80]
[80] Ama yule kijana niliye muuwa, baba yake na mama yake walikuwa ni Waumini. Tulikuwa tunajua kuwa angeli ishi angeli kuwa ndio sababu ya ukafiri wao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na ama mvulana niliyemuua alikuwa, katika ujuzi wa Allah Mtukufu, ni kafiri, na baba yake na mama yake walikuwa Waumini, tukaogopa lau huyu mvulana ataendelea kuishi atawatia wazazi wake kwenye ukafiri na udhalimu wenye kupita kiasi kwa kumpenda kwao au kwa kumuhitajia.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net