Al-Kahf 18:51
الكهفمَّآ أَشْهَدتُّهُمْ خَلْقَ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ وَلَا خَلْقَ أَنفُسِهِمْ وَمَا كُنتُ مُتَّخِذَ ٱلْمُضِلِّينَ عَضُدًا
Sikuwashuhudisha kuumbwa kwa mbingu na ardhi, wala kuumbwa kwa wao wenyewe. Wala sikuwafanya wapotezao kuwa ni wasaidizi.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Sikuwashuhudisha kuumbwa kwa mbingu na ardhi, wala kuumbwa kwa nafsi zao. Wala sikuwafanya wapotezao kuwa ni wasaidizi. [51]
[51] Mimi sikumwonyesha Iblisi wala dhuriya zake nilipo umba mbingu wala ardhi, wala sikuwashuhudisha baadhi yao nilipo waumba wenzao ili wanisaidie. Wala sikuwa nina haja ya msaidizi wowote, licha kuwa nikatafute wapotovu ndio wawe wasaidizi wangu. Basi yawaje mnakwenda mt'ii Shetani na mkaniasi Mimi?
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Sikumleta Iblisi na kizazi chake, ambao nyinyi mnawatii, katika uumbaji wa mbingu na ardhi, nikataka msaada wao kuziumba, wala sikuwashuhudisha baadhi yao uumbaji wa wengine. Bali mimi nilipwekeka katika kuumba zote hizo bila msaidizi wala mwenye kutilia nguvu, na sikuwa ni mwenye kuwafanya wapotezaji miongoni mwa Mashetani na wengineo kuwa ni wasaidizi, basi vipi nyinyi mnawapatia haki yangu na mnawafanya wao ni wategemewa wenu badala yangu na hali mimi ndiye muumba wa kila kitu.?
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net