Al-Kahf 18:50
الكهفوَإِذْ قُلْنَا لِلْمَلَـٰٓئِكَةِ ٱسْجُدُوا۟ لِـَٔادَمَ فَسَجَدُوٓا۟ إِلَّآ إِبْلِيسَ كَانَ مِنَ ٱلْجِنِّ فَفَسَقَ عَنْ أَمْرِ رَبِّهِۦٓ ۗ أَفَتَتَّخِذُونَهُۥ وَذُرِّيَّتَهُۥٓ أَوْلِيَآءَ مِن دُونِى وَهُمْ لَكُمْ عَدُوٌّۢ ۚ بِئْسَ لِلظَّـٰلِمِينَ بَدَلًا
Na tulipowaambia Malaika: Msujudieni Adam! Wakamsjudia isipokuwa Iblisi. Yeye alikuwa miongoni mwa majini, na akavunja amri ya Mola wake Mlezi. Je, mnamchukua yeye na dhuria yake kuwa vipenzi badala yangu, hali wao ni adui zenu? Ni ovu mno badala hii ya madhalimu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na tulipo waambia Malaika: Msujudieni Adam! Walimsjudia isipo kuwa Iblisi. Yeye alikuwa miongoni mwa majini, na akavunja amri ya Mola wake Mlezi. Je! Mnamshika yeye na dhuriya zake kuwa marafiki badala yangu, hali wao ni adui zenu? Ni ovu mno badala hii kwa wenye kudhulumu. [50]
[50] Ewe Mtume! Watajie mwanzo wa kuumbwa kwao, ili wajue kuwa wao wametokana na udongo, basi wasikae wakidanganyika na hayo waliyo nayo, wakamnyenyekea Iblisi, adui wa baba yao. Kwani yeye alikuwa katika majini, akajivuna, na akamuasi Mwenyezi Mungu. Basi yawaje baada ya kwisha jua khabari zake mkamfanya yeye na kizazi chake kuwa ndio wasaidizi wenu badala ya Mwenyezi Mungu. Na hao ndio adui zenu! Badala hii ni ovu kwa mwenye kuidhulumu nafsi yake na akamt'ii Shetani.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na kumbuka pale tulipowaamrisha Malaika kumsujudia Ãdam, kimaamkizi na sio kiibada, na tukamwamrisha Iblisi vile tulivyowaamrisha Malaika. Hapo Malaika wote walisujudu, lakini Iblisi aliyekuwa ni miongoni mwa majini, alitoka nje ya utiifu wa Allah Mtukufu na asisujudu kwa kiburi na wivu. Basi mnamfanya yeye, enyi watu, na waliozalikana na yeye kuwa ni wasaidizi wenu, mkawa mnawatii na mnaacha kunitii mimi, na hali yeye ni adui yenu aliye mtesi mno? Ni ubaya ulioje wa madhalimu kumtii Shetani badala ya kumtii Mwingi wa rehema.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net