Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 18 · Aya ya 49

Al-Kahf 18:49

الكهف

وَوُضِعَ ٱلْكِتَـٰبُ فَتَرَى ٱلْمُجْرِمِينَ مُشْفِقِينَ مِمَّا فِيهِ وَيَقُولُونَ يَـٰوَيْلَتَنَا مَالِ هَـٰذَا ٱلْكِتَـٰبِ لَا يُغَادِرُ صَغِيرَةً وَلَا كَبِيرَةً إِلَّآ أَحْصَىٰهَا ۚ وَوَجَدُوا۟ مَا عَمِلُوا۟ حَاضِرًا ۗ وَلَا يَظْلِمُ رَبُّكَ أَحَدًا

Maana

Na kitawekwa mbele Kitabu. Basi utawaona wahalifu wanavyoogopa mno kwa sababu ya yale yaliyomo. Na watasema: "Ole wetu! Kitabu hiki kina nini! Hakikuacha dogo wala kubwa isipokuwa kililidhibiti vyema?" Na watayakuta yote waliyoyatenda yapo hadharani. Na Mola wako Mlezi hamdhulumu yeyote.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na kitawekwa kitabu. Basi utawaona wakosefu wanavyo ogopa kwa yale yaliomo humo. Na watasema: Ole wetu! Kitabu hichi kina nini! Hakiachi dogo wala kubwa ila huliandika? Na watayakuta yote waliyo yatenda yamehudhuria hapo. Na Mola wako Mlezi hamdhulumu yeyote. [49]

[49] Na katika mkono wa kila mmojapo kitawekwa kitabu cha vitendo vyake. Waumini watakiona na watafurahi kwa yaliyomo humo. Na wakanushaji wataona nao wamejaa khofu kwa vitendo viovu viliomo humo. Watasema wakisha ona hayo: Hilaki gani hii! Tunastaajabia kitabu hichi hakikuacha hata dogo katika vitendo vyetu, wala kubwa, ila kimetuandikia! Na wataona malipo ya waliyo yatenda ni ya haki. Wala Mola wako Mlezi hamdhulumu yeyote katika waja wake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na kitawekwa kitabu cha matendo ya kila mtu kuliani kwake au kushotoni kwake, hapo utawaona waasi wameingiwa na hofu kwa yaliyomo ndani kwa sababu ya mambo ya uhalifu waliyoyafanya, na watasema watakapokiangalia, «Ewe maangamivu yetu! Kina nini kitabu hiki hakikuacha dogo wala kubwa isipokuwa kimelisajili?» Na watayakuta yote waliyoyafanya ulimwenguni yako mbele yao yamesajiliwa. Na Mola wako Hamdhulumu yoyote hata kadiri ya chungu mdogo. Mtiifu hatapunguziwa malipo yake mema, na muasi hataongezewa mateso yake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Kahf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net