Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 18 · Aya ya 48

Al-Kahf 18:48

الكهف

وَعُرِضُوا۟ عَلَىٰ رَبِّكَ صَفًّا لَّقَدْ جِئْتُمُونَا كَمَا خَلَقْنَـٰكُمْ أَوَّلَ مَرَّةٍۭ ۚ بَلْ زَعَمْتُمْ أَلَّن نَّجْعَلَ لَكُم مَّوْعِدًا

Maana

Na wakahudhurishwa mbele ya Mola wako Mlezi kwa safu (wakaambiwa): Mmetujia kama tulivyowaumba mara ya kwanza! Bali mlidai kwamba hatutawawekea miadi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wakahudhurishwa mbele ya Mola wako Mlezi kwa safu (wakaambiwa): Mmetujia kama tulivyo kuumbeni mara ya kwanza! Bali mlidai kwamba hatutakuwekeeni miadi. [48]

[48] Na Siku hii watu watahudhurishwa kwa makundi wakipangwa kwa masafu kwa ajili ya hisabu. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu atasema: Tumekufufueni kutokana na mauti, kama tulivyo kuumbeni pale mara ya mwanzo. Na mmetujia peke yenu, mmoja, mmoja, bila ya mali, na bila ya wana. Na duniani mlikuwa mkikanusha kufufuliwa na kuhisabiwa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na hapo watahudhurishwa wote kwa Mola wako wakiwa wamejipanga safu, hakuna yoyote kati yao anayefichwa, na hapo Awaambie «Tumewafufua na mumetujia mkiwa peke yenu, hamna mali wala watoto, kama vile tulivyowaumba mara ya kwanza. Bali mlifikiria kwamba hatutawawekea nyinyi wakati wa kuwafufua na kuwalipa kwa matendo yenu».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Kahf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net