Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 18 · Aya ya 47

Al-Kahf 18:47

الكهف

وَيَوْمَ نُسَيِّرُ ٱلْجِبَالَ وَتَرَى ٱلْأَرْضَ بَارِزَةً وَحَشَرْنَـٰهُمْ فَلَمْ نُغَادِرْ مِنْهُمْ أَحَدًا

Maana

Na siku tutakapoiondoa milima na ukaiona ardhi iwazi, na tukawafufua, wala hatutamwacha hata mmoja miongoni mwao.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na siku tutapo iondoa milima na ukaiona ardhi iwazi, na tukawafufua - wala hatutamwacha hata mmoja kati yao [47]

[47] Na ewe Mtume! Waonye watu kwa Siku ambayo vyote viliopo vitaondoka. Milima itaondoka, na mtaiona ardhi tupu wazi imetanda, hapana chochote kilicho kuwapo cha kuisitiri. Na tutawafufua watu kwa ajili ya hisabu, na hatutamwacha hata mmoja kati yao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wakumbushe Siku tutakapoyaondoa majabali kutoka mahali pake, na ukaiona ardhi waziwazi haina vya kufunika miongoni mwa viumbe vilivyokuwa juu yake, na tukawakusanya wa mwanzo na wa mwisho kwenye kisimamo cha kuhesabiwa, tusimuache yoyote miongoni mwao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Kahf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net