Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 18 · Aya ya 52

Al-Kahf 18:52

الكهف

وَيَوْمَ يَقُولُ نَادُوا۟ شُرَكَآءِىَ ٱلَّذِينَ زَعَمْتُمْ فَدَعَوْهُمْ فَلَمْ يَسْتَجِيبُوا۟ لَهُمْ وَجَعَلْنَا بَيْنَهُم مَّوْبِقًا

Maana

Na siku atakaposema (Mwenyezi Mungu): Waiteni hao mliodai kuwa ni washirika wangu. Basi watawaita, na wao hawatawaitikia. Nasi tutaweka baina yao maangamio.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na siku atakapo sema (Mwenyezi Mungu): Waiteni hao mlio dai kuwa ni washirika wangu. Basi watawaita, na wao hawato waitikia. Nasi tutaweka baina yao maangamio. [52]

[52] Watajie siku atayo waambia Mwenyezi Mungu washirikina: Waiteni hao mlio kuwa mkidai duniani kuwa ni washirika wangu katika ibada ili wakuombeeni kwa mujibu wa madai yenu. Nao watawaita, na hao hawato waitikia. Nasi tumejaalia sasa hapana baina yao ila ni maangamizo tu kwa makafiri, baada ya kuwa duniani walikuwa na mawasiliano ya ibada na mapenzi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na wakumbushe pindi Atakaposema Allah Mtukufu kuwaambia washirikina Siku ya Kiyama, «Waiteni washirika wangu ambao mlikuwa mnadai kwamba wao ni washirika wangu katika ibada, wapate kuwaokoa na mimi leo.» Hapo wataomba uokozi wao, na wao wasiwaokoe, na tutaweka baina ya wenye kuabudu na waabudiwa kitu cha kuwaangamiza katika moto wa Jahanamu wawe wote ni wenye kuangamia humo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Kahf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net