Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 18 · Aya ya 43

Al-Kahf 18:43

الكهف

وَلَمْ تَكُن لَّهُۥ فِئَةٌ يَنصُرُونَهُۥ مِن دُونِ ٱللَّهِ وَمَا كَانَ مُنتَصِرًا

Maana

Wala hakuwa na kikundi cha kumnusuru badala ya Mwenyezi Mungu, wala mwenyewe hakuweza kujinusuru.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wala hakuwa nacho kikundi cha kumsaidia badala ya Mwenyezi Mungu, wala mwenyewe hakuweza kujisaidia. [43]

[43] Katika balaa hii hakuwa na jamaa wa kuja mnusuru badala ya Mwenyezi Mungu kama alivyo kuwa akijitapa. Wala hakuwa anaweza kujisaidia nafsi yake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na hakuwa na kundi la watu, kati ya wale ambao alijifahiri nao, wenye kumtetea na adhabu ya Allah Mtukufu yenye kumshukia, wala hakuwa ni mwenye kujitetea kwa nafsi yake na nguvu zake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Kahf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net