Al-Kahf 18:44
الكهفهُنَالِكَ ٱلْوَلَـٰيَةُ لِلَّهِ ٱلْحَقِّ ۚ هُوَ خَيْرٌ ثَوَابًا وَخَيْرٌ عُقْبًا
Huko ulinzi ni wa Mwenyezi Mungu wa Haki tu. Yeye ndiye mbora zaidi wa malipo, na wa mwisho ulio bora zaidi.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Huko ulinzi ni wa Mwenyezi Mungu wa Haki tu. Yeye ndiye mbora wa malipo, na mbora wa matokeo. [44]
[44] Kwani katika kila hali nusura iko kwa Mwenyezi Mungu wa Haki peke yake. Na Yeye Subhanahu ni Mwema kwa mja wake Muumini, humkirimu kwa malipo, na humfanyia mema matokeo yake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Katika shida kama hizi mategemeo na usaidizi huwa uko kwa Allah Mtukufu wa haki. Yeye ni bora wa kulipa mema na ni bora wa kuwapa mwisho mwema wale walioko hifadhini Mwake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net