Al-Kahf 18:42
الكهفوَأُحِيطَ بِثَمَرِهِۦ فَأَصْبَحَ يُقَلِّبُ كَفَّيْهِ عَلَىٰ مَآ أَنفَقَ فِيهَا وَهِىَ خَاوِيَةٌ عَلَىٰ عُرُوشِهَا وَيَقُولُ يَـٰلَيْتَنِى لَمْ أُشْرِكْ بِرَبِّىٓ أَحَدًا
Basi, yakateketezwa matunda yake, akabaki akipinduapindua viganja vyake, kwa vile alivyoyagharamia, huku miti yake imebwagika juu ya chanja zake. Akawa anasema: Laiti nisingelimshirikisha Mola wangu Mlezi na yeyote!
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Yakateketezwa matunda yake, akabaki akipindua pindua viganja vyake, kwa vile alivyo yagharimia, na miti imebwagika juu ya chanja zake. Akawa anasema: Laiti nisingeli mshiriki Mola wangu Mlezi na yeyote! [42]
[42] Mwenyezi Mungu kampatiliza yule kafiri, akayateketeza mavuno yote ya kitalu chake, na hicho kitalu chenyewe akakiangamiza, na akang'oa hata mizizi yake. Yule kafiri akabakia akipindua pindua viganja vyake kwa kusikitikia gharama alizo zitoa katika kukiamirisha kitalu chake, na baadae kuja kikapatilizwa na uharibifu. Akatamani lau kuwa hakumshirikisha Mola wake Mlezi na yeyote.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Yakawa ni kweli yale maneno ya yule Muumini, na shamba likaharibika na vilivyomo ndani vikaangamia, akawa yule kafiri anageuza vitanga vyake vya mikono huku na huku kwa kulilia hasara na majuto kwa gharama aliyoitoa pale, na hali miti yake imeanguka chini baadhi yake iko juu ya mingine, na akawa yuwasema, «Natamani lau ningezitambua neema za Allah Mtukufu na uwezo Wake na sikumshirikisha Allah Mtukufu na yoyote.» Na haya ni majuto yake wakati ambapo majuto hayamfalii kitu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net