Al-Kahf 18:4
الكهفوَيُنذِرَ ٱلَّذِينَ قَالُوا۟ ٱتَّخَذَ ٱللَّهُ وَلَدًا
Na kiwaonye wasemao, "Mwenyezi Mungu alijifanyia mwana."
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na kiwaonye wanao nena: Mwenyezi Mungu ana mwana. [4]
[4] Na kiwaonye kwa njia makhsusi wale walio msingizia Mwenyezi Mungu kuwa ana mwana, na hali Yeye ametakasika kuwa kama viumbe, akawa mwenye kuzaa au akazaliwa mtoto wake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na awaonye kwayo washirikina waliosema, «Allah Mtukufu Amejifanyia mtoto».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net