Al-Kahf 18:5
الكهفمَّا لَهُم بِهِۦ مِنْ عِلْمٍ وَلَا لِـَٔابَآئِهِمْ ۚ كَبُرَتْ كَلِمَةً تَخْرُجُ مِنْ أَفْوَٰهِهِمْ ۚ إِن يَقُولُونَ إِلَّا كَذِبًا
Wao hawana elimu yoyote ya jambo hili, wala baba zao. Ni neno kubwa hilo litokalo vinywani mwao. Hawasemi isipokuwa uongo tu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wao hawana ujuzi wa jambo hili, wala baba zao. Ni neno kuu hilo litokalo vinywani mwao. Hawasemi ila uwongo tu. [5]
[5] Wala wao hawana ujuzi wowote wa hayo wala baba zao hawakuwa nao huo. Ni uzushi mkubwa mno huu wa kutoa neno hili vinywani mwao! Wayasemayo ni uzushi, na wala hapana uzushi mkubwa kushinda huu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hawa washirikina hawana ujuzi wowote wa kile wanachokidai kwamba Allah Mtukufu Amejifanyia mtoto, vilevile wale waliopita kabla yao ambao wao wamewaiga, hawakuwa na ujuzi huo. Ni makubwa sana maneno haya mabaya yanayotoka kwenye vinywa vyao. Wao hawasemi isipokuwa urongo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net