Al-Kahf 18:39
الكهفوَلَوْلَآ إِذْ دَخَلْتَ جَنَّتَكَ قُلْتَ مَا شَآءَ ٱللَّهُ لَا قُوَّةَ إِلَّا بِٱللَّهِ ۚ إِن تَرَنِ أَنَا۠ أَقَلَّ مِنكَ مَالًا وَوَلَدًا
Na lau kuwa ulipoingia kitaluni kwako, ungelisema: Mashaallah (alitakalo Mwenyezi Mungu huwa)! Hakuna nguvu yoyote isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu. Ikiwa unaniona mimi nina mali kidogo zaidi na watoto kuliko wewe.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na lau kuwa ulipo ingia kitaluni kwako ungeli sema: Mashaallah! Alitakalo Mwenyezi Mungu huwa! Hapana nguvu ila kwa Mwenyezi Mungu. Ikiwa unaniona mimi nina mali kidogo na watoto kuliko wewe, [39]
[39] Na lau kuwa ungeli sema unapo ingia katika hii bustani yako ya duniani na ukaangalia viliomo ndani yake: Haya Mashaallah! Ndio aliyo yataka Mwenyezi Mungu. Wala mimi sina nguvu ya kuyapata haya bila ya msaada wa Mwenyezi Mungu. Hayo inge kuwa ni shukrani za kupelekea kudumu neema yako. Tena akazidi kumwambia: Ikiwa umeniona mimi ni duni kuliko wewe kwa mali na watoto na wasaidizi...
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kwani si ingalikuwa afadhali, ulipoingia kwenye shamba lako na likakupendeza, kama ungemshukuru Allah Mtukufu na ukasema, ‘Haya ni yale aliyonitakia Allah Mtukufu, sina nguvu ya kuyapata isipokuwa ni kwa Allah Mtukufu.’ Iwapo waniona mimi kuwa ni mchache wa mali na watoto kuliko wewe.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net