Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 18 · Aya ya 38

Al-Kahf 18:38

الكهف

لَّـٰكِنَّا۠ هُوَ ٱللَّهُ رَبِّى وَلَآ أُشْرِكُ بِرَبِّىٓ أَحَدًا

Maana

Lakini Yeye Mwenyezi Mungu ndiye Mola wangu Mlezi. Wala simshirikishi Mola wangu Mlezi na yeyote.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Lakini Yeye Mwenyezi Mungu ndiye Mola wangu Mlezi. Wala simshirikishi na yeyote. [38]

[38] Lakini mimi ninasema: Hakika aliye niumba mimi na akaumba ulimwengu wote huu ni Mwenyezi Mungu Mola wangu Mlezi. Na mimi namuabudu Yeye peke yake, wala simshirikishi na yeyote.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Lakini mimi sisemi maneno hayo yako yanayoonyesha ukafiri wako. Kwa kweli, mimi nasema ‘Mwenye kuneemesha na kufanya hisani ni Allah Mtukufu Mola wangu Peke Yake, na mimi simshirikishi yeye katika kumuabudu na yoyote asiyekuwa Yeye.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Kahf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net