Al-Kahf 18:37
الكهفقَالَ لَهُۥ صَاحِبُهُۥ وَهُوَ يُحَاوِرُهُۥٓ أَكَفَرْتَ بِٱلَّذِى خَلَقَكَ مِن تُرَابٍ ثُمَّ مِن نُّطْفَةٍ ثُمَّ سَوَّىٰكَ رَجُلًا
Mwenzake akamwambia kwa kubishana naye: Je, unamkufuru aliyekuumba kutokana na udongo, tena kutokana na tone la manii, kisha akakufanya mwanamume aliye sawasawa?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Mwenzake akamwambia kwa kubishana naye: Je! Unamkufuru aliye kuumba kutokana na udongo, tena kutokana na tone la manii, kisha akakufanya mtu kaamili? [37]
[37] Mwenzie Muumini akamjibu: Unajiachilia kumkufuru Mola wako Mlezi aliye kuumba tangu asli yako ya Adam kutokana na udongo, kisha kutokana na tone ya maji-maji ya mbegu ya uzazi, kisha akakufanya mtu aliye kamilika? Ikiwa unajiona bora kwa mali yako na jamaa zako, basi mkumbuke Mola wako Mlezi na asli yako ya udongo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Mwenzake Muumini akamwambia, huku akimjadili kwa kumuwaidhia, «Vipi wewe utamkanusha Allah Mtukufu Aliyekuumba kwa mchanga kisha kwa tone la manii kisha Akakusawazisha kwa kukufanya binadamu mwenye kimo kilicholingana na umbo?» Katika aya hii pana dalili ya kwamba mwenye uwezo wa kuanzisha kuumba viumbe ni muweza wa kuwarudisha.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net