Al-Kahf 18:36
الكهفوَمَآ أَظُنُّ ٱلسَّاعَةَ قَآئِمَةً وَلَئِن رُّدِدتُّ إِلَىٰ رَبِّى لَأَجِدَنَّ خَيْرًا مِّنْهَا مُنقَلَبًا
Wala sidhani kuwa hiyo Saa (ya Kiyama) itatokea. Na ikiwa nitarudishwa kwa Mola wangu Mlezi, bila ya shaka nitapata marejeo bora zaidi kuliko haya.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wala sidhani kuwa hiyo Saa (ya Kyama) itatokea. Na ikiwa nitarudishwa kwa Mola wangu Mlezi, bila ya shaka nitapata marejeo bora zaidi kuliko haya. [36]
[36] Wala sidhani kuwa Kiyama kitakuja. Na pindi ikawa nikirejea kwa Mola wangu Mlezi kwa kufufuliwa kama unavyo dai wewe, basi Wallahi! Hapana shaka nitapata bustani bora kuliko kitalu hiki huko Akhera. Kwani mimi ni mtu wa neema kwa kila hali. Yeye huyu anakisia hayo ya ghaibu kwa haya yaliyoko sasa. Wala hajui kuwa Akhera malipo yake ni kwa Imani na vitendo vya kheri.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na siamini kwamaba Kiyama ni chenye kutokea, na kikitokea kwa kukisia tu, kama unavyodai ewe mwenye kuamini, na nikarudishwa kwa Mola wangu, basi huko Kwake nitapata bora zaidi kuliko shamba hili nirudishiwe na nirejeshewe, kwa ajili ya utukufu wangu na cheo changu Kwake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net