Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 18 · Aya ya 40

Al-Kahf 18:40

الكهف

فَعَسَىٰ رَبِّىٓ أَن يُؤْتِيَنِ خَيْرًا مِّن جَنَّتِكَ وَيُرْسِلَ عَلَيْهَا حُسْبَانًا مِّنَ ٱلسَّمَآءِ فَتُصْبِحَ صَعِيدًا زَلَقًا

Maana

Basi huenda Mola wangu Mlezi akanipa kilicho bora kuliko kitalu chako, na akakitumia balaa kutoka mbinguni kwa hivyo kikageuka kuwa ardhi tupu inayoteleza.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi huenda Mola wangu Mlezi akanipa kilicho bora kuliko kitalu chako, naye akapitisha kudra yake kutoka mbinguni kukilitea hicho chako, na kikageuka ardhi tupu inayo teleza. [40]

[40] ...basi huenda Mola wangu Mlezi akanipa bora kuliko hiyo bustani yako, hapa duniani au kesho Akhera, na akaipelekea bustani yako kudra yake aliyo ikadiria, kama radi mathalan kutoka mbinguni. Na ikawa ardhi kavu inayo teleza haimei kitu, wala unyayo hautulii juu yake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Basi Allah Mtukufu huenda Akanipa mimi bora zaidi kuliko shamba lako, na Akakuondolea hiyo neema kwa ukafiri wako, na akailetea shamba lako adhabu kutoka mbinguni ikawa ni ardhi tupu iliyo kavu ambayo nyayo haziwezi kuthibiti juu yake wala hakuna mmea unaoota.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Kahf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net