Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 18 · Aya ya 30

Al-Kahf 18:30

الكهف

إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ إِنَّا لَا نُضِيعُ أَجْرَ مَنْ أَحْسَنَ عَمَلًا

Maana

Hakika wale walioamini na wakatenda mema, hakika Sisi hatupotezi ujira wa anayetenda mazuri.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hakika wale walio amini na wakatenda mema - hakika Sisi hatupotezi ujira wa anaye tenda mema. [30]

[30] Ama wale walio muamini Mwenyezi Mungu na Dini ya Haki uliyo funuliwa wewe, na wakatenda aliyo waamrisha Mola wao Mlezi, nayo ni vitendo vyema, basi Sisi hatuto wapotezea ujira wao wa vitendo vyema walivyo vitenda.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika wale waliomuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na wakafanya matendo mema watakuwa na malipo makubwa kabisa. Sisi hatupotezi malipo yao wala hatutawapunguzia kwa matendo mazuri waliyoyafanya.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Kahf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net